• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 29, 2021

  SALAH AKOSA PENALTI, LIVERPOOL YAPIGWA 1-0


  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah jana alikosa penalti Liverpool ikichapwa bao 1-0 na wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power.
  Mkwaju wa penalti wa Salah ulipanguliwa na kipa Kasper Schmeichel dakika ya 15 na alipojaribu kuunganisha mpira uliorudi ukagonga mwamba.
  Bao pekee la Leicester City lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Everton, Ademola Lookman dakika ya 59 na kwa ushindi huo katika mchezo wa 18 wanafikisha pointi 25 katika nafasi ya tisa.
  Kwa upande wao Liverpool wanabaki na pointi zao 41 katika nafasi ya pili, sawa na Chelsea ya tatu, wote wakiwa nyuma ya mabingwa watetezi,  Manchester City baada ya timu zote kucheza mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAH AKOSA PENALTI, LIVERPOOL YAPIGWA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top