• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  SALAH AIFUNGIA BAO PEKEE LA USHINDI LIVERPOOL


  BAO pekee la Liverpool la mshambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah kwa penalti dakika ya 67 limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Pamoja na ushindi huo, Liverpool inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake 37, ilizidiwa moja na Manchester City baada ya wote kucheza mechi 16, wakati Aston Villa ya kocha Steven Gerrard inabaki na pointi zake 19 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAH AIFUNGIA BAO PEKEE LA USHINDI LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top