• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  RONALDO AING’ARISHA MANCHESTER UNITED ENGLAND


  TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Carrow Road.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Cristiano Ronaldo kwa penalti dakika ya 75 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Aarons, huo ukiwa mwendelezo mzuri kwa kocha mpya, Mjerumani, Ralf Rangnick.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 27 katika nafasi ya tano, ikizidiwa wastani wa mabao tu na West Ham United inayoshika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 16, wakati Norwich City inabaki na pointi zake 10 mkiani mwa ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AING’ARISHA MANCHESTER UNITED ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top