• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 09, 2021

  RANGNICK ABADILI KIKOSI CHOTE MAN U YATOA SARE


  TIMU ya Manchester United imekamilisha mechi zake za Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sare ya 1-1 na Young Boys Uwanja wa Old Trafford.
  Mason Greenwood alianza kuwafungia wenyeji, Manchester United dakika ya tisa, kabla ya Fabian Rieder kuisawazishia Young Boys dakika ya 42.
  Man United wanamaliza na pointi 11 kileleni mwa kundi wakifuatiwa na Villarreal yenye pointi saba na zote zinafuzu ya 16 Bora zikizipiku Atalanta iliyomaliza na pointi sita na Young Boys pointi tano.
  Kocha mpya, Mjerumani Ralf Rangnick aliingia na mabadiliko ya wachezaji 11 kikosini, akiwaanzisha Amad Diallo na Anthony Elanga kwenye safu ya ushambuliaji na kipindi cha pili akawaingiza KIPA Tom Heaton pamoja na Charlie Savage na Zidane Iqbal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RANGNICK ABADILI KIKOSI CHOTE MAN U YATOA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top