• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 22, 2021

  NKETIAH AIPELEKA ARSENAL NUSU FAINALI CARABAO


  WENYEJI, Arsenal wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Sunderland usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Shujaa wa Arsenal jana alikuwa ni mshambuliaji Eddie Nketiah aliyefunga mabao matatu peke yake dakika za 17, 49 na 58, wakati mabao mengine yamefungwa na Nicolas Pepe dakika ya 27 na kinda wa umri wa miaka 18 aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza, Charlie Patino dakika ya 90 na ushei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NKETIAH AIPELEKA ARSENAL NUSU FAINALI CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top