• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 13, 2021

  NI VITA YA MESSI NA RONALDO TENA ULAYA


  TIMU ya Manchester United itamenyana na Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Mabingwa watetezi, Chelsea watavaana na timu nyingine ya Ufaransa, Lille.
  Katika droo iliyopangwa leo Jijini Nyon nchini Uswisi, timu nyingine za England, Liverpool itamenyana na FC Red Bull Salzburg ya Austria na Manchester City itavaana na Villarreal ya Hispania.
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 15, 16, 22 na 23 na marudiano Machi 8,9,15 na 16 mwakani.
  Mechi kati ya Manchester United na PSG zinatarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee zikiwakutanisha tena wanasoka wapinzani wakubwa, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.


  RATIBA KAMILI 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA
  Benfica vs Real Madrid 
  Villarreal vs Man City 
  Atletico vs Bayern 
  Salzburg vs Liverpool 
  Inter vs Ajax 
  Sporting vs Juventus 
  Chelsea vs Lille 
  PSG vs Man Utd
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI VITA YA MESSI NA RONALDO TENA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top