• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 19, 2021

  MARTINELLI APIGA MBILI ARSENAL YAUA 4-1


  WENYEJI, Leeds United wamechapwa mabao 4-1 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Elland Road mjini Leeds, West Yorkshire.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Martinelli mawili dakika ya 16 na 28, Bukayo Saka dakika ya 42 na Emile Smith Rowe dakika ya 84, wakati la Leeds United limefungwa na Raphinha kwa penalti dakika ya 75.
  Arsenal inafikisha pointi 32 baada ya ushindi huo na kujiweka sawa nafasi ya nne, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 16 katika nafasi ya 16 baada ya wote kucheza mechi 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARTINELLI APIGA MBILI ARSENAL YAUA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top