• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 13, 2021

  MAN UNITED SASA NA ATLETICO 16 BORA ULAYA

  TIMU ya Manchester United sasa itamenyana na Atletico Madrid badala ya Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  UEFA ilibaini dosari kadhaa katika droo ya awali iliyopangwa mchana wa leo Jijini Nyon nchini Uswisi na kuamua kuirudia jioni hii na ndipo Man United ilipotenganishwa na PSG.
  Mabingwa watetezi, Chelsea wao droo mpya imewaachia mpinzani yule yule, Lille ya Ufaransa, wakati timu nyingine za England, Liverpool sasa itamenyana na Inter Milan ya Italia badala ya FC Red Bull Salzburg ya Austria na Manchester City sasa itavaana na Sporting Lisbon ya Ureno badala ya Villarreal ya Hispania.
  Mechi kati ya Manchester United na PSG ilitarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kwa sababu ingewakutanisha tena wanasoka wapinzani wakubwa, Cristiano Robaldo na Lionel Messi.
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 15, 16, 22 na 23 na marudiano Machi 8,9,15 na 16 mwakani.


  RATIBA MPYA 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA
  RB Salzburg v Bayern Munich
  Sporting Lisbon v Manchester City
  Benfica v Ajax
  Chelsea v Lille
  Atletico Madrid v Manchester United 
  Villarreal v Juventus 
  Inter Milan v Liverpool
  PSG v Real Madrid
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED SASA NA ATLETICO 16 BORA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top