• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 30, 2021

  MAN CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamezidi kuwaacha mbali wapinzani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford City usiku wa Jumatano Uwanja wa Brentford Community, Brentford, Middlesex.
  Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, Phil Foden dakika ya 16 akimalizia kazi nzuri ya Kevin de Bruyne kumchambua kipa Alvaro Fernandez.
  Ushindi huo unaifanya Manchester City imalize mwaka kileleni mwa Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 50, nane zaidi ya mabingwa wa Ulaya, Chelsea wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi 20.


  Kikosi cha kocha Pep Guardiola pia kinauingia mwaka 2022 na rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo za Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top