• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 05, 2021

  MAN CITY YAIPIGA WATFORD 3-1 NA KUPAA KILELENI


  TIMU ya Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Watford mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vicarage.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nne na Bernardo Silva mawili dakika ya 31 na 63, wakati la Watford limefungwa na mtokea benchi, Cucho Hernandez dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Man City ya kocha Pep Guardiola inafikisha pointi 35 na kupanda kileleni mwa ligi, ikiizidi pointi moja Liverpool inayofuatia na mbili Chelsea, wakati Watford inabaki na pointi zake 13 katika nafasi ya 17 baada ya timu zote kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIPIGA WATFORD 3-1 NA KUPAA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top