• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  MAN CITY YAICHAPA WOLVES 1-0 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Raheem Sterling kwa penalti ya utata dakika ya 66, hilo likiwa bao lake la 100 katika Ligi Kuu ya England.
  Wolves ilimaliza pungufu baada ya Raul Jimenez kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Man City wanafikisha pointi 38 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool inayocheza mechi yake ya 16 muda huu dhidi ya Aston Villa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA WOLVES 1-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top