• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 26, 2021

  MAN CITY YAICHAPA LEICESTER 6-3 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wameendelea kufurahia matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 6-3 dhidi ya wenyeji, Leicester City jioni ya leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya tano, Riyad Mahrez kwa penalti dakika ya 14, İlkay Gündoğan dakika ya 21, Raheem Sterling mawili, moja kwa penalti dakika ya 25 na lingine dakika ya 87 akimalizia pasi ya Rúben Dias na Aymeric Laporte dakika ya 69.
  Kwa upande wao, Leicester City mabao yao yamefungwa na James Maddison dakika ya 55, Ademola Lookman dakika ya 59 na Kelechi Iheanacho dakika ya 65 ambaye pia ndiye mpishi wa mabao mengine yote mawili.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 44 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 18, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 22 za mechi 16 katika nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA LEICESTER 6-3 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top