• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 15, 2021

  MAN CITY YAIBAMIZA LEEDS UNITED 7-0


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Leeds United mabao 7-0 usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Phil Foden dakika ya nane, Jack Grealish dakika ya 13, Kevin De Bruyne mawili dakika ya32 na 62, Riyad Mahrez dakika ya 49, John Stones dakika ya 74 na mtokea benchi, Nathan Ake dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 41 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA LEEDS UNITED 7-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top