• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 08, 2021

  MAN CITY YACHAPIKA UJERUMANI 2-1


  TIMU ya Manchester City jana imechapwa mabao 2-1 na wenyeji, RB Leipzig katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig.
  Mabao ya RB Leipzig yalifungwa na Dominik Szoboszlai dakika ya 24 na Andre Silva dakika ya 71, wakati la Man City limefungwa na Riyad Mahrez dakika ya 76. 
  Manchester City ilimaliza pungufu baada ya Kyle Walker kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 82 kwa kumchezea rafu, Andre Silva.
  Lakini Manchester City inamaliza kileleni mwa Kundi A ikiwa na pointi 12, moja zaidi ya PSG na zote zimefuzu Hatua ya 16 Bora, wakati RB Leipzig imemaliza na pointi saba, mbili zaidi ya Club Brugge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YACHAPIKA UJERUMANI 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top