• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 08, 2021

  LIVERPOOL YAWEKA REKODI MPYA YA USHINDI ULAYA


  TIMU ya Liverpool imeendeleza wimbi la ushindi kwa asilmia 100 katika Ligi yaMabingwa Ulaya baada ya kuwachapa wenyeji, AC Milan mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi B usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, Italia.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah dakika ya 36 na Divock Origi dakika ya 55, wakati bao pekee la Milan limefungwa na beki wa zamani wa Chelsea, Fikayo Tomori dakika ya 28.  
  Liverpool inakuwa timu ya kwanza ya England kushinda mechi zote sita za makundi za Ligi ya Mabingwa ikimaliza na pointi 18 ikifuatiwa na Atletico Madrid pointi saba na zote zimetinga Hatua ya 16 Bora zikizipiku Porto iliyomaliza na pointi sita na AC Milan pointi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAWEKA REKODI MPYA YA USHINDI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top