• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 23, 2021

  LIVERPOOL YAITOA LEICESTER KWA MATUTA CARABAO


  TIMU ya Liverpool imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 3-3 na Leicester City usiku huu Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Leicester City yamefungwa na mshambuliaji mkongwe, Jamie Vardy mawili, dakika ya tisa na 13 na James Maddison dakika ya 33, wakati ya Liverpool yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 19, Diogo Jota dakika ya 68 na Takumi Minamino dakika ya 90 na ushei.
  Katika mikwaju ya penalti, sifa zimuendee kipa wa pili wa Liverpool, Caoimhin Kelleher aliyeokoa mikwaju miwili ya wachezaji wa Leicester City, Luke Thomas na Ryan Bertrand.
  Minamino pekee alikosa penalti upande wa Liverpool, wakati wote, James Milner, Roberto Firmino, Oxlade-Chamberlain, Naby Keïta  na wote walifunga.
  Waliofunga Penalti za Leicester City ni Youri Tielemans, James Maddison, Marc Albrighton na Kelechi Iheanacho na sasa Wekundu hao watakutana na ama Tottenham, Chelsea au Arsenal katika Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITOA LEICESTER KWA MATUTA CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top