• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 17, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 3-1


  WENYEJI, Liverpool usiku wa jana wamewatandika Newcastle United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 21, Mohamed Salah dakika ya 25 na Trent Alexander-Arnold dakika ya 87 baada ya Newcastle kutangulia kwa bao la Jonjo Shelvey dakika ya saba.
  Liverpool inafikisha pointi 40, lakini inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 17.
  Hali inazidi kuwa mbaya kwa Newcastle United ikibaki na pointi zake 10, yaani inaizidi tu wastani wa mabao Norwich City inayoshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top