• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 19, 2021

  LIVERPOOL PUNGUFU YATOA SARE NA SPURS 2-2 LONDON


  WENYEJI, Tottenham Hotspur wamelazimishwa sare ya 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Spurs yamefungwa na Harry Kane dakika ya 13 na Son Heung-Min dakika ya 74, wakati ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 35 na Andy Robertson dakika ya 69 kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakka ya 77 kwa kumchezea rafu Emerson Royal.
  Liverpool inafikisha pointi 40 na kubaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18, wakati Tottenham inatimiza pointi 26 za mechi 15 katika nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL PUNGUFU YATOA SARE NA SPURS 2-2 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top