• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 07, 2021

  EVERTON YAICHAPA ARSENAL 2-1 GOODISON PARK


  WENYEJI, Everton wametoka nyuma na kuwachapa Arsenal 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.
  Martin Odegaard alianza kuifungia Arsenal dakika ya 45, kabla ya Richarlison kuisawazishia Everton dakika ya 79 na Demarai Gray kufunga la ushindi dakika ya 90 na ushei.
  Ben Godfrey alinusurika kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga tele usoni Takehiro Tomiyasu na bahati zaidi kwao Arsenal mabao mengine mawili ya Richarlison yalikataliwa.
  Everton inafikisha pointi 18 kwa ushindi huo na kusogea nafasi ya 12, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 23 katika nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi nane.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EVERTON YAICHAPA ARSENAL 2-1 GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top