• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  ETO’O RAIS MPYA WA SOKA YA CAMEROON  MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o ameshinda nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka nchini mwake, (FECAFOOT) jana nchini humo.
  Mwanasoka huyo Bora wa Afrika, alipata kura 43 dhidi ya 31 za Seidou Mbombo Njoya, aliyeingia madarani mwaka 2018.
  Baada ya ushindi huo, nyota huyo wa zamani wa Barcelona mwenye umri wa miaka 40 sasa, alisema; “Nimefurahi mno kuchaguliwa kama Rais mpya,".
  "Kila kura inawakilisha nguvu na dhamira ya familia yetu ya soka, kuupeleka mchezo wetu pendwa katika kiwango ambacho haikwahi kuonekana kabla," aliongeza Eto'o mshindi wa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili akiwa na Barca na moja na Inter Milan.
  Cameroon watakuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kuanzia Januari 9 hadi Februari 7, mwakani.
  Akiwa anacheza, Eto’o aliiwezesha Indomitable Lions kushinda mataji mawili ya AFCON na Medali ya Dhahabu ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2000.
  Amekuwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.
  Amechezea kwa mafanikio klabu za Real Madrid, Leganés, Espanyol, Mallorca, Barcelona za Hispania, Inter Milan ya Italia, Anzhi Makhachkala ya Urusi, Chelsea, Everton za England, Sampdoria ya Italia, Antalyaspor, Konyaspor za Uturuki na 13 Qatar SC ya Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO’O RAIS MPYA WA SOKA YA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top