• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  CHELSEA YAZINDUKA, YAILAZA LEEDS UNITED 3-2

  TIMU ya Chelsea imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England ndani ya wiki sita baada ya kuichapa Leeds United 2-2 usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Mason Mount dakika ya 42 na Jorginho mawili yote kwa penalti dakika ya 58 na 90 na ushei, wakati ya Leeds yamefungwa na Raphinha kwa penalti pia dakika ya 28 na kinda Joe Gelhardt dakika ya 83.
  Chelsea inafikisha pointi 36 katika nafasi ya tatu, nyuma ya Manchester City pointi 38 na Liverpool 37 baada ya wote kucheza mechi 16, wakati Leeds inabaki na pointi zake 16 nafasi ya 15 ikiwa imecheza mechi 16 pia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAZINDUKA, YAILAZA LEEDS UNITED 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top