• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 05, 2021

  CHELSEA YAPOROMOSHWA KILELENI ENGLAND


  WENYEJI, West Ham wameichapa Chelsea mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Thiago Silva dakika ya 28 na Mason Mount dakika ya 44, wakati ya West Ham yamefungwa na Manuel Lanzini kwa penalti dakika ya 44, Jarrod Bowen dakika ya 56 na Arthur Masuaka dakika ya 87.
  Ushindi huo unaifanya West Ham ya kocha David Moyes iifikishe pointi 27 na kusogea nafasi ya nne ikizidiwa pointi sita na Chelsea baada ya mechi 15 kwa wote na The Blues inaangukia nafasi ya tatu kutoka kileleni ilipodumu kwa muda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAPOROMOSHWA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top