• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 17, 2021

  CHELSEA YALAZIMISHWA SARE, 1-1 NA EVERTON DARAJANI


  WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya 1-1 na Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Mason Mount alianza kuifungia Chelsea dakika ya 70 kabla ya chipukizi, Jarrad Branthwaite kuisawazishia Everton dakika ya 74 na kwa sare hiyo The Blues inafikisha pointi 37 ikibaki nafasi ya tatu ikiwa inazidiwa na pointi tatu na Liverpool baada ya wote kucheza mechi 17.
  Everton kwa upande wao baada ya sare hiyo wanafikisha pointi 19 katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 20 baada ya kucheza mechi 17 pia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE, 1-1 NA EVERTON DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top