• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 27, 2021

  CHELSEA YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 VILLA PARK


  TIMU ya Chelsea imeonyesha kuimarika tena baada ya ushindi wa ugenini wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Reece James alianza kujifunga dakika ya 28 kuipatia Aston Villa bao la kwanza, kabla ya Chelsea kuzinduka kwa mabao ya Jorginho , mawili na yote kwa penalti dakika ya 34 na 90 na ushei na mtokea benchi, Romelu Lukaku dakika ya 56.
  Kwa ushindi huo, The Blues wanafikisha pointi 41 katika mchezo wa 19, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, wakizidiwa tu wastani wa mabao na Liverpool ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Aston Villa ambayo ilicheza bila kocha wake,  Steven Gerrard ambaye aliwekwa kando baada ya vipimo kuonyesha ameabukizwa virusi vya  corona, inabaki na pointi zake 22 za mechi 18 katika nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top