• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 30, 2021

  CHELSEA YACHOMOLEWA DAKIKA YA MWISHO DARAJANI


  WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brighton & Hove Albion usiku wa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Chelsea ilitangulia kwa bao la Romelu Lukaku dakika ya 28, kabla ya Danny Welbeck kuisawazishia Brighton dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 20, ikisogea nafasi ya pili ikiwa inaizidi pointi moja tu Liverpool ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi na timu hizo zitamenyana Jumapili katika mechi ya kuwania nafasi ya pili.
  Manchester City ndio inaongoza mbio za ubingwa kwa mbali, ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 20 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YACHOMOLEWA DAKIKA YA MWISHO DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top