• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 19, 2021

  CHELSEA YAAMBULIWA SARE KWA WOLVES MOLINEUX


  TIMU ya Chelsea imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Molineux.
  Chelsea ililazimishwa kucheza mechi hiyo baada ya kuomba ombi lake kutaka iahirishwe kutokana na kukabiliwa na wagonjwa wengi wa COVID 19 kukataliwa.
  Chelsea inafikisha pointi 38 na kuendelea kushika nafasi ya tatu sasa ikiizidi pointi sita tu Arsenal, wakati Wolves inafikisha pointi 25 katika nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi 18.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIWA SARE KWA WOLVES MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top