• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 28, 2021

  CAVANI ATOKEA BENCHI KUINUSURU KIPIGO MAN UNITED


  MSHAMBULIAJI mkongwe wa Uruguay, Edison Cavani ametokea benchi usiku wa Jumatatu na kuifungia bao la kusawazisha Manchester United ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Newcastle United Uwanja wa St James' Park.
  Cavani alifunga bao hilo dakika ya 71 baada ya kuingia mwanzoni tu mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa England, Mason Greenwood.
  Newcastle ilitangulia kwa bao la mapema tu, dakika ya saba la kiungo Mfaransa, Allan Saint-Maximin.
  Mashetani Wekundu walikuwa kando la ligi kwa siku 16 kutokana na kukabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji waliokuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
  Kwa sare hiyo, Man United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 17 ikiwa nafasi ya saba, wakati Newcastle ya kocha Muingereza, Eddie Howe imetimiza pointi ya 11 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAVANI ATOKEA BENCHI KUINUSURU KIPIGO MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top