• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 09, 2021

  BARCA YAKWAMA MAKUNDI BAADA YA MIAKA 21


  WENYEJI, Bayern Munich wameichapa Barcelona 3-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani.
  Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Thomas Muller dakika ya 34, Leroy Sane dakika ya 43 na Jamal Musiala dakika ya 62.
  Kwa matokeo hayo, Bayern Munich inamaliza na pointi 18 kileleni mwa kundi hilo, ikifuatiwa na Benfica pointi nane na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora.
  Kwa pointi zake saba, Barcelona inamaliza nafasi ya tatu mbele ya Dynamo Kiev yenye pointi moja na kutupwa nje ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza wakishindwa kuvuka hatua ya makundi ndani ya miaka 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCA YAKWAMA MAKUNDI BAADA YA MIAKA 21 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top