• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 26, 2021

  ARSENAL YAWAPA ZAWADI YA 5-0 MASHABIKI WAKE


  TIMU ya Arsenal imewapa zawadi nzuri mashabiki wake jioni ya leo baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya wenyeji, Norwich City FC Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, Norfolk.
  Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Bukayo Saka mawili, dakika ya sita na 67, Kieran Tierney dakika ya 44, Alexandre Lacazette kwa penalti dakika ya 84 na Emile Smith Rowe dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 32, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa pointi sita na Chelsea, baada ya timu zote kucheza mechi 18, wakati Norwich inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi zake 10 za mechi 17 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWAPA ZAWADI YA 5-0 MASHABIKI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top