• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 16, 2021

  ARSENAL YAPANDA ‘TOP FOUR’ ENGLAND


  WENYEJI, Arsenal wamefanikiwa kupanda nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United usiku huu Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya The Gunners yamefungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 48 na mtokea benchi, Emile Smith Rowe dakika ya 78 na kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 29 na kupanda nafasi ya nne ikiizidi pointi moja West Ham kufuatia timu zote kucheza mechi 17.
  Wagonga Nyundo wa London, West Ham walimaliza pungufu baada ya Vladimir Coufal kutolewa Kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Alexandre Lacazette kwenye boksi na mkwaju wa penalti wa Mfaransa huyo ukaokolewa na kipa Mpoland, Łukasz Fabianski dakika ya 69.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPANDA ‘TOP FOUR’ ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top