• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 12, 2021

  ARSENAL YAITANDIKA SOUTHAMPTON 3-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 21, Martin Odegaard dakika ya 27 na 
  Gabriel Magalhães dakika ya 62 katika mchezo ambao kocha Mikel Arteta alimuanzishia benchi Nahodha, Pierre-Emerick Aubameyang.
  Arsenal inafikisha pointi 26 katika nafasi ya sita, ikiizidi pointi 10 Southampton inayoshika nafasi ya 16 baada ya timu zote kucheza mechi 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAITANDIKA SOUTHAMPTON 3-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top