• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 07, 2021

  WEST HAM YAICHAPA LIVERPOOL 3-2 LONDON


  WENYEJI, West Ham United wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London.
  Mabao ya West Ham la kwanza alijifunga kipa Alisson Becker dakika ya nne, la pili Pablo Fornals dakika ya 67 na Kurt Zouma dakika ya 74, wakati ya Liverpool yamefungwa na Trent Alexander-Arnold dakika ya 41 na Divock Origi dakika ya 83.
  West Ham inafikisha pointi 23 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi pointi moja Liverpool na ikizidiwa wastani wa mabao tu na Manchester City na wote wakiwa nyuma ya Chelsea inayoongoza kwa pointi tatu zaidi baada ya wote kucheza mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WEST HAM YAICHAPA LIVERPOOL 3-2 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top