• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 20, 2021

  WATFORD YAICHAPA MAN UNITED 4-1


  WENYEJI, Watford wameiadhibu Manchester United kwa kipigo cha 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road, Watford.
  Mabao ya Watford yamefungwa na Josh King dakika ya 28, Ismailia Sarr dakika ya 48, Joao Pedro dakika ya 90 na ushei na dakika tatu baadye Emmanuel Dennis akafunga la nne, wakati mtokea benchi Donny van de Beek ndiye mfungaji wa bao pekee la United dakika ya 50.
  Kipigo hicho cha tano cha msimu kinaifanya Manchester United iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Harry Maguire kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 69 ibaki na pointi zake 17 baada ya mechi saba katika nafasi ya saba.
  Kwa upande wao, Watford ya kocha Claudio Ranieri inatimiza pointi 13 baada ya kucheza mechi 13 katika nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WATFORD YAICHAPA MAN UNITED 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top