• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 12, 2021

  UJERUMANI YAUA 9-0 KOMBE LW DUNIA


  TIMU ya taifa ya Ujerumani imeibuka na ushindi wa 9-0 dhidi ya Liechtenstein katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia barani Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa VOLKSWAGEN ARENA Jijini Wolfsburg.
  Thomas Muller na Leroy Sane kila mmoja alifunga mabao mawili, wakati mabao mengine yamefungwa na Ilkay Gundogan kwa penalti, Daniel Kaufmann na Maximilian Göppel waliojifunga, Marco Reus na Ridle Baku.
  Wageni walilazimika kucheza 10 tangu dakika ya tisa baada ya Jens Hofer kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Leon Goretzka.
  Tayari Ujerumani imefuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia Qatar ikiongoza Kundi J kwa pointi zake 24, tisa zaidi ya Macedonia Kaskazini wanaofuatia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAUA 9-0 KOMBE LW DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top