• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 15, 2021

  RONALDO ASHINDWA KUIPELEKA URENO QATAR


  NYOTA Cristiano Ronaldo jana alishindwa kuisaidia Ureno kupata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia baada ya kuchapwa 2-1 nyumbani na Serbia Uwanja wa Luz Jijini Lisbon.
  Renato Sanches aliyeanza badala ya Bruno Fernandes aliifungia bao la kuongoza Ureno dakika ya pili, kabla ya Dusan Tadic kuisawazishia Serbia dakika ya 33 na Aleksandar Mitrovic kufunga la ushindi dakika ya 90.
  Serbia inamaliza na pointi 20 kileleni kwa Kundi A na kufuzu moja kwa moja Kombe la Dunia, mwakani wakati Ureno ya Cristiano Ronaldo iliyoshika nafasi ya pili kwa pointi zake 17 itakwenda Play-Offs kujaribu bahati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO ASHINDWA KUIPELEKA URENO QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top