• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 03, 2021

  RONALDO AINUSURU MAN UNITED KUCHAPWA ULAYA


  BAO la dakika ya mwisho la Cristiano Ronaldo usiku wa Jumanne limeisaidia Manchester United kupata sare ya 2-2 na wenyeji, Atalanta katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Gewiss mjini Bergamo.
  Josip Illicic alianza kuifungia Atalanta dakika ya 12, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia United dakika ya 45 na ushei.
  Duvan Zapata akawafungia la pili wenyeji, Atalanta dakika ya 56, kabla ya Ronaldo kuisawazishia tena United dakika ya 90 na ushei.
  Kwa sare hiyo, United inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza Kundi F kwa wastani wa mabao tu dhidi ya Villarreal, wakati Atalanta imefikisha pointi tano na Young Boys yenye pointi tatu inashika mkia baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AINUSURU MAN UNITED KUCHAPWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top