• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 21, 2021

  MESSI AFUNGA BAO LA KWANZA UFARANSA


  MSHAMBULIAJI Lionel Messi jana amefunga bao lake la kwanza Ligue 1, Ufaransa akiiwezesha Paris Saint-Germain kuichapa 3-1 Nantes Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris.
  Messi alifunga bao la tatu dakika ya 87 akimalizia pasi ya Kylian Mbappe aliyefunga pia bao la kwanza dakika ya pili tu, wakati bao la pili Dennis Appiah alijifunga dakika ya 81.
  Bao pekee la Nantes lilifungwa na Randal Kolo Muani dakika ya 76 katika mchezo huo ambao PSG ilimaliza pungufu baada ya Keylor Navas kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AFUNGA BAO LA KWANZA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top