• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 28, 2021

  MAN CITY YAICHAPA WEST HAM 2-1


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 33 na Fernandinho dakika ya 90, wakati la West Ham limefungwa na mtokea benchi, Manuel Lanzini dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 29 na kurejea nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi mbili na vinara, Chelsea wakati West Ham inabaki na pointi zake 23 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA WEST HAM 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top