• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 21, 2021

  LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL 4-0


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumamosi Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Wekundu wa Anfield yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 39, Diogo Jota dakika ya 52, Mohamed Salah dakika ya 73 na Takumi Minamino dakika ya 77.
  Liverpool imefikisha pointi 25 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya pili ilizidiwa pointi nne na vinara, Chelsea baada ya wote kucheza mechi 12, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 20 za mechi 12 pia nafasi ya  tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top