• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 27, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA SOUTHAMPTON 4-0


  WENYEJI Liverpool wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield leo.
  Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na mshambuliaji Mreno, Diogo Jota mawili dakika ya pili na 32, kiungo Mspaniola, Thiago Alcรขntara dakika ya 37 na beki Mholanzi, Virgil van Dijk dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, kikosi cha kinafikisha pointi 28 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya pili, kikizidiwa pointi moja na vinara, Chelsea ambao pia wana mechi moja mkononi. Southampton inabaki na pointi zake 14 za mechi 13 nafasi ya 14. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA SOUTHAMPTON 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top