• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 03, 2021

  LEWANDOWSKI APIGA HAT TRICK BAYERN YASHINDA 5-2


  WENYEJI, Bayern Munich wameibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Benfica katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mshambuliaji Mpoland, Robert Lewandowski amefunga mabao matatu peke yake akicheza mechi yake ya 100 Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Lewandowski alifunga dakika ya 26, 61 na 84, huku pia akikosa penalti dakika ya 45, wakati mabao mengine ya Bayern Munich yamefungwa na Serge Gnabry dakika ya 32 na Leroy Sane dakika ya 49 huku ya Benfica yalifungwa na Morato dakika ya 38 na Darwin Nunez dakika ya 74.
  Kwa ushindi huo, Bayern Munich imefikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza Kundi E, ikifuatiwa kwa mbali na Barcelona yenye pointi sita, Benfica nne, Dinamo Kiev moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LEWANDOWSKI APIGA HAT TRICK BAYERN YASHINDA 5-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top