• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 15, 2021

  KAPTENI AYEW AIPELEKA GHANA QATAR


  BAO pekee la Nahodha, Andre Ayew dakika ya 33 kwa penalti jana limeipa Ghana ushindi wa 1-0 dhidi ya Afrika Kusiki katika mchezo wa mwisho wa Kundi G kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa Cape Coast mjini Cape Coast.
  Ghana na Afrika Kusini zote zinamaliza na pointi 13 kila moja katika kundi hilo, lakini Black Stars wanakwenda hatua ya mwisho ya mchujo wa safari ya Qatar barani kwa wastani mzuri zaidi wa mabao, kwani wao wamefunga mabao saba, moja zaidi ya Bafana Bafana.
  Timu nyingine zilizofuzu hatua ya mwisho ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mali, Misri, Senegal na Morocco kuelekea mechi za mwisho leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAPTENI AYEW AIPELEKA GHANA QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top