• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 13, 2021

  KANE APIGA HAT TRIC ENGLAND YAUA 5-0


  ENGLAND imebisha hodi Qatar baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Albania katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mabao ya Three Lions yamefungwa na Harry Kane matatu dakika za 18, 33 na 45 na mengine Harry Maguire dakika ya tisa na Jordan Henderson dakika ya 28.
  Kwa ushindi huo, Three Lions wanafikisha pointi 23 na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Poland, wakati Albania yenye pointi 15 ni ya tatu baada ya wote kucheza mechi tisa.
  Sasa England watahitaji pointi moja tu katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi I dhidi ya San Marino Jumatatu ili kujikatia tiketi ya Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KANE APIGA HAT TRIC ENGLAND YAUA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top