• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 17, 2021

  CAMEROON NA TUNISIA ZAFUZU, IVORY COAST NJE KOMBE LA DUNIA


  TIMU za Cameroon na Tunisia zimekamilisha idadi ya timu 10 za kwenda hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia kwa kanda ya Afrika baada ya ushindi katika mechi zao za jana.
  Simba Wasiofungika wameitoa Ivory Coast kwa ushindi wa 1-0 Jijini Yaounde na kumaliza kileleni mwa Kundi D, wakati Tunisia imeifunga Zambia 3-1 Jijini Rades kumaliza kileleni mwa Kundi B.
  Bao pekee la Cameroon lilifungwa na Karl Toko Ekambi dakika ya 21, wakati mabao ya Tunisia yalifungwa na Aissa Laidouni dakika ya 18, Mohamed Drager dakika ya 30 na Ali Maaloul dakika ya 43 na la Zambia lilifungwa na Fashion Sakala dakika ya 80.
  Cameroon na Tunisia zinaungana na Morocco, Misri, Nigeria, Algeria, Mali, Senegal, Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Sasa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litapanga ratiba ya mechi tano baina ya timu hizo kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON NA TUNISIA ZAFUZU, IVORY COAST NJE KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top