• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 24, 2021

  BAYERN YASHINDA, BARCA DROO


  TIMU ya Bayern Munich imeendeleza ubabe baada ya kuwachapa wenyeji, Dynamo Kiev 2-1 katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa NSK Olimpiki Jijiji Kiev nchini Ukraine.
  Mabao ya Bayern Munich usiku wa jana yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 14 na Kingsley Coman dakika ya 42, wakati la Dinamo Kiev lilifungwa na Denys Harmash dakika ya 70.


  Mechi nyingine ya kundi hilo, FT
  Barcelona chini ya kocha mpya, Xavi ililazimishwa sare ya 0-0 na Benfica Uwanja wa Camp Nou.
  Bayern Munich ambayo tayari imeshafuzu Hatua ya 16 Bora inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Barcelona yenye pointi saba, Benfica tano na Dinamo Kiev moja.
  Barcelona italazimika kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Bayern Munich Desemba 8 Ujerumani ili kwenda Hatua ya 16 Bora au kuwaombea mabaya Benfica wafungwe na Dinamo Kiev kwenye mechi ya mwisho Ureno.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAYERN YASHINDA, BARCA DROO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top