• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 12, 2021

  SENEGAL YATANGULIZA MGUU MMOJA QATAR


  MSHAMBULIAJI wa Alanyaspor ya Uturuki, Famara Diédhiou amefunga mabao yote matatu, Senegal ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji wahamiaji, Namibia katika mchezo wa Kundi H leo Uwanja wa Orlando Stadium Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Mpachika mabao huyo wa zamani wa Bristol City ya England alifunga mabao hayo dakika za 22,61 na 84, wakati bao pekee la Namibia limefungwa na mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Peter Shalulile dakika ya 27.
  Kwa ushindi hui, Simba wa Teranga wanafikisha pointi 12 na kufuzu hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar kuelekea mechi mbili za mwisho za kundi hilo.
  Senegal wanafuatiwa na Togo na Namibia zenye pointi nne kila moja na Kongo yenye pointi mbili baada ya mechi nne wote, maana yake hata wakishinda mechi zao zilizosalia wataishia kwenye pointi 10.
  Senegal sasa itasubiri kumenyana na mmoja wa washindi wa makundi mengine tisa na wakishinda watakwenda tena Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SENEGAL YATANGULIZA MGUU MMOJA QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top