• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 10, 2021

  MADAGASCAR YAICHAPA DRC 1-0


  WENYEJI, Madagascar wamepata ushindi wa kwanza katika Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuwachapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 1-0 usiku wa leo Uwanja wa Munispaa ya Mahamasina Jijini Antananarivo.
  Bao pekee la Madagascar leo limefungwa na kiungo wa Fleury ya Ufaransa, Njiva Tsilavina Martin Rakotoharimalala dakika ya pili tu ya mchezo huo wa mzunguko wa nne.
  Pamoja na ushindi huo, Madagascar inaendelea kushika mkia Kundi J kwa pointi zake tatu, nyuma ya DRC yenye pointi tano na Benin na Tanzania zenye pointi saba kila moja baada ya mechi nne.
  Mechi mbili za mwisho, Madagascar itawafuata Benin Novemba 11 kabla ya kuwaalika Tanzania siku tatu baadaye Antananarivo.
  Na DRC watakuwa wageni wa Tanzania Novemba 11, kabla ya kuwakaribisha Benin siku tatu baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MADAGASCAR YAICHAPA DRC 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top