• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 10, 2021

  VIHIGA QUEENS WATWAA KOMBE LA MAMA SAMIA

  WENYEJI, Vihiga Queens wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa wanawake, maarufu kama CECAFA Women’s Samia Cup baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Commercial Bank ya Ethiopia jana Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi, Kenya.
  Shujaa wa Vihiga jana alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Gentrix Shikangwa aliyefunga mabao yote mawili, la pili kwa penalti dakika ya mwisho, wakati Vivian Makokha alijifunga kuwapa bao la kufutia machozi Wahabeshi.
  Kwa ushindi huo, pamoja na kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, Vihiga pia wamepata dola za Kimarekani 30, 000 sehemu ya dola 100,000 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.


  Commercial Bank wamepata dola 20,000 na Lady Doves WFC ya Uganda iliyoshika nafasi ya tatu baada ya kuichapa Simba Queens 2-1 pia jana mchana hapo hapo Kasarani imepata dola 10,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIHIGA QUEENS WATWAA KOMBE LA MAMA SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top