• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 03, 2021

  ALGERIA YAICHAPA DJIBOUTI 8-0 BLIDA


  TIMU ya taifa ya Algeria imeanza kwa kishindo mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Djibouti katika mchezo wa Kundi A jana Uwanja wa Mustapha Tchaker Jijini Blida.
  Mshambuliaji wa Lyon ya Ufaransa, Islam Slimani peke yake alifunga mabao manne jana dakika ya tano, 25 kwa penalti, 46 na 53.
  Mengine yamefungwa na washambuliaji Ramy Bensebaini wa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani dakika ya 26, Baghdad Bounedjah wa Al Sadd ya Qatar kwa penalti dakika ya 40, Riyad Mahrez wa Manchester City dakika ya 67 na kiungo wa FC Twente ya Uholanzi, Ramiz Larbi Zerrouki dakika ya 69. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALGERIA YAICHAPA DJIBOUTI 8-0 BLIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top