• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 11, 2021

  RAJA CASABLANCA WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  KLABU ya Raja Casablanca ya Morocco imetwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria usiku wa jana Uwanja wa Uwanja wa de l'Amitié Jijini Cotonou, Cameroon.
  Mabao ya Raja yalifungwa na washambuliaji Soufiane Rahimi dakika ya tano na Mkongo Ben Malango Ngita dakika ya 14, kabla ya Mohammed Zakaria Boulahia kuifungia Kabylie la kufutia machozi dakika ya 46.
  Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafuatia Jumamosi ijayo baina ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAJA CASABLANCA WATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top